pembetatu ya Bermuda (Bermuda triangle) na maajabu yake



Pembetatu ya Bermuda (Bermuda Triangle) ni eneo katika Bahari ya Atlantiki ikiwa inapakana na Florida ,Bermuda na Puertorico ambalo ni eneo la tarkibani km700,000. Sehemu ambapo meli na ndege nyingi zimepata kupotea katika mazingira tatanishi sana kiasi kwamba wanasayansi wameshindwa kuelezea kwa kina na kujikuta akisema pana maajabu yasiyoelezeka na hii ndio sababu ya kujulikana kama devil's triangle yaani pembetatu ya shetani 

VYOMBO AMBAVYO VIMESHAWAHI POTEA BERMUDA
  •  U.S Navy bomber Katika mazingira ya kutatanisha july1945 U.S Navy bombers tano zilizokua zimebeba watu 14 zikitokea Fort Lauderdale. Hizi zilikuwa zimepelekwa huko kwa ajili ya mazoezi na wanajeshi ila cha kushangaza zilikutwa zimetelekezwa. Inasadikiwa kwamba Compas ya kiongozi wa msafara huo ilishindwa kufanya kazi na wenyewe kujikuta wamepotea baada ya kuzunguka na kuishiwa mafuta na hata hivyo ndege iliyotumwa kwa ajili ya uokozi na yenyewe ilipotea ikiwa na watu 13 ndani. waliwatafuta bila mafaniio na mwishoni wakahitimisha kwamba ilipotea kana kwamba immeelekea sayari ya Mars.
  • ndege tano za U.S Navy zilizopotea july1945
  Flight 19   5dec 1945 ndege ya mafunzo ya warusha mabomu ya TM AVENGER ilitoweka ikiwa juu ya bahari ya antlantiki,taarifa za mawasiliano ya mwisho kati ya marubanina wanaanga wa marekani zilijulisha kuwa hali ya hewa ilikuwa ya dhoruba katika bahari licha ya kutokuonyesha tatizo lolote la usumaku wa dunia                                                                        
  • KC-135 Stratotanker mnamo 28Agosti1963 ndege za kivita za marekani zilizitangazwa zimegogangana katika bahari ya antlantiki, lakini ukweli kutokana na utafiti uliofanyika na Kusche kutokana na uchunguzi uliofanyika na AIR FORCE hizi ndege mbili hazikugongana kwani zilikuwa umbali wa maji takribani kilometa 260 hii ni baada ya uchunguzi wa mabaki yaliyopatikana
  • S.V.SPRAY.
  • ilikuwa mashua ilioundwa kama meli na Joshua slocum ambayo alitumia kuzungukia ulimwengu mnamo mwaka1895-1898. Mnamo mwaka 1905 Slocum aling'oa nanga kutoka kutoka Vineyard Heaven kwenda Venezuela akiwa safarini  mashua hii haikupatikana wala Slocum mwenyewe hajawahi onekana tena.
  • Vyombo vingine ni pamoja na meli ya Mary Celeste, meli ya SS EL Faro iliozama 1octoba2015 ,na vijana wawili Austin Stephanos na Perry Cohen waliokuwa wakivua samaki eneo la Bermuda mnamo july2015 
  •  
                                                                                                                                                                                           
WADAU WANAIONGELEAJE BERMUDA 
  • Sehemu hii inayoitwa pembe tatu ya bemuda au pembe tatu ya shetani (Devil’s Triangle) ina ukubwa wa laki tano squire miles ya eneo la bahari upande wa kusini mashariki wa jimbo la Florida marekani. kwa wanahistorial wanamklumbuka mtu mmoja aliyejulikana kwa jina la Christopher Columbus yeye anasema kwamba wakati amefika maeneo haya kwa mara ya kwanza ambapo inasemekana yeye ndio aliyegundua eneo la marekani aliripoti kwamba aliona moto mkubwa ukidondoka eneo hilo na inasadikika kwamba ni kimondo. Anaendelea kwamba baada ya wiki kadhaa palitokea mwanga flani ambao yeye hakuelewa ni wa kitu gani ila wajuzi wa jiografia wanadai ni kimondo hicho. Pamoja na hayo amezungumzia masuala ya kusoma kompasi , ila wadau pia wakasema ni kwa kuwa eneo hilo ndipo kwa kipindi hicho ndipo sehemu chache Duniani ambapo True North na Magnetic North zinapita kwa pamoaja. Hapa kwa wanajiografia wanaelewa zaidi.
  •  mfululizo wa kupotea baadhi ya vyombo na vingine kukutwa vimetelekezwa ndio hasa unaowatisha watu kuhusu eneo hilo. Tangu mnamo mwaka 1964 jina la "pembtetatu ya Bermuda" lilibuniwa na kusambazwa na waandishi wa habari wakijaribu kueleza kupotea kwa boti, meli na ndege katika eneo hili. Kitabu cha Berlitz cha mwaka 1974 "The Bermuda Triangle ( kiliuzwa mara milioni na kusambaza habari za eneo lililoaminiwa kuwa na hatari za pekee.
  • Inadaiwa kutoweka kwa ndege na meli katika hali isiyojulikana ambayo haiwezi kuelezewa kama makosa ya binadamu, uharamia, hitilafu ya vifaa, au au maafa ya kiasili. Tamaduni maarufu zinahusisha kutoweka huku na jambo lisilo la kawaida ambalo haliwezi kuelezewa kwa njia za kisayansi, kutanguliwa kwa sheria za fizikia, au shughuli za viumbe visivyo vya kawaida (Alliens). Nyaraka nyingi hufunua, hata hivyo, kwamba sehemu kubwa ya madai ya matukio haya ya kidude hayajaripotiwa kwa makini au baadaye kurembeshwa na waandishi, na mashirika mbalimbali rasmi yamesema kwamba idadi na aina ya kutoweka katika eneo hili ni sawa na eneo lolote la bahari.
  viumbe vinavyosadikika kuwepo bermuda(alliens)

Maoni

Chapisha Maoni